Washukiwa watano wanaohusishwa na shambulio la Jumanne la hoteli ya Dusit mjini Nairobi wamewasilishwa mahakamani .
Watano hao ni pamoja na raia mmoja wa Canada.
Mahakama iliruhusu upande wa mashtaka kuwaweka rumande kwa siku 30 huku uchunguzi ukiendelea.
Takriban watu 21 waliuawa wakati wapiganaji walipovamia hoteli ya DusitD2 .
Wanaume wanne walisimamishwa kizimbani katika mahakama kuu jijini Nairobi huku wakificha nyuso zao.
Ni washukiwa wa kwanza kufikishwa mahakamani wakihusishwa na shambulio hilo baya katika hoteli ya DusitD2, lakini hawakusomewa mashtaka yao.
Mkurugenzi wa mashtaka ametaka kupewa muda zaidi ili kufanya uchunguzi alioutaja kuwa mgumu na wa kimataifa.
Chanzo:Bbc
0 comments:
Post a Comment