Na. Mwandishi wetu. Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza waamuzi watakaochezesha mechi ya Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba na JS Saoura. Waamuzi hao ni Joshua Bondo ambaye atasimama kama mwamuzi wa kati, waamuzi wasaidizi Oamogetse Godisamang, Moemedi Godfrey Monakwane na mwamuzi wa akiba, Kutlwano Leso, wote kutoka nchini Botswana. Kamishna wa mechi ni James Leonard Mwenda kutoka nchini Malawi, msimamizi mkuu wa mchezo huo ni Alexander Sakyi Asante kutoka nchini Ghana. Simba itawakaribisha JS Saoura katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi ambao utapigwa Januari 12 Jijini Dar…
0 comments:
Post a Comment