Mwanamasumbwi, Manny Pacquiao kutoka Ufipino ameshinda pambano lake dhidi ya Mmarekani Adrien Broner kwa points (Unanimous Decision) na kufanikiwa kutetea ubingwa wake wa WBA Welterweight.
Pambano hilo lilifanyika Mjini Las Vegas, Marekani asubuhi ya kuamkia leo, Majaji wote watatu wamempa Pacquiao pointi 117-111, 116-112, 116-112.
Pacquiao (40) alimzidi Broner kwenye karibia raundi zote 12, jambo ambalo limefanya apate ushindi huo kiurahisi.
Baada ya pambano hilo, Pacquiao alimtumia salamu Bondia mwenzake Floyd Mayweather kwa kumwambia kuwa akubali warudie pambano lingine.
“Mwambieni (Mayweather) arudi ulingoni, mimi nipo tayari kupambana naye.” amesema Pacquiao ambaye mwaka 2015 alipigwa na Bondia huyo .
Tazama pambano la jana hapa chini
0 comments:
Post a Comment