Wednesday, 9 January 2019

UPINZANI WAONYA MATOKEO YA UCHAGUZI NCHINI DRC

...
Mgombea wa urais wa upinzani nchini Congo DRC Martin Fayulu amewaonya maafisa wa uchaguzi dhidi ya ''kuficha ukweli'' huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda baada ya matokeo ya uchaguzi kucheleweshwa.

Bwana Fayulu amesema watu wa Congo tayari wanajua  matokeo ya uchaguzi uliyofanyika Desemba 30 kuahirishwa kwa wiki moja.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yalitarajiwa kutangazwa siku ya Jumapili ya Januari 6 lakini yakaahirishwa.

Uchaguzi huo ulikuwa wa kumtafuta mrithi wa rais Joseph Kabila, ambaye anaachia madaraka baada ya kuongoza nchi hiyo ya maziwa makuu kwa miaka 18.

Kabila ameahidi kwamba uchaguzi huo ambao ulikuwa umepangwa ufanyike miaka miwili uliyopita utakuwa wa kwanza wa kupokezana madaraka kwa njia ya kidemokrasia nchini DR Congo tangu taifa hilo lilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1960.

Mrithi wake anayempendelea ambaye pia ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Shadary,anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wagombea wa upinzani Martin Fayulu,tajiri mkubwa wa mafuta na Felix Tshisekedi, mwana wa kiume wa kigogo wa upinzani.

Chanzo:Bbc
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger