Friday, 18 January 2019

TCRA yatoa leseni 224 za watoa huduma za maudhui mtandaoni...93 ni za Blogs, 97 ni za Online Tv

...
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema leseni 224 zimetolewa kwa watoa huduma za maudhui mtandaoni kati ya Machi na Desemba 2018.

Kati ya leseni hizo, 93 ni kwa wamiliki wa blogs, majukwaa ya majadiliano mtandaoni mawili, redio mtandao 32, televisheni mtandao 97.

Kilaba ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) inayofanyika katika ofisi za TCRA jijini Dar es Salaam.

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao na kujihakikishia kuwa maudhui yanayotolewa yanakuwa sahihi.

“TCRA haizuii matumizi ya mitandao ya kijamii katika utoaji wa maudhui bali tunalinda maslahi mapana na endelevu ya jamii inayotumia huduma hizo hususani watoto,” amesema Kilaba.

Amesema kutokana na hali hiyo hivi sasa Watanzania wanapata taarifa ya habari bure kupitia chaneli za ndani kwa mujibu wa sheria.


from MPEKUZI http://bit.ly/2HjwHYj
via Malunde
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger