Wizara ya nishati kupitia wakala wa umeme vijijini (REA) wamewasha umeme kwenye vijiji sita vilivyopo wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani ikiwa ni mradi wa ujazilizi wenye malengo ya kuwakwamua wananchi kiuchumi. Akizungumza kwenye ziara hiyo naibu waziri wa nishati Mhe Subira Mgalu amesema kuwa mradi huo wa ujazilizi ambao umeunganisha umeme kwenye vijiji sita wilayani Kisarawe ni utekelezaji wa serikali katika kuhakikisha wananchi wote wanapata nishati hiyo muhimu kwa ajili ya maisha yao na maendeleo kwa ujumla huku akisema kauli mbiu ya ‘zima kibatari’. “Tumewasha umeme kwenye vijiji hivi sita…
0 comments:
Post a Comment