Friday, 4 January 2019

SERIKALI KUMTUMIA SAMATTA KUTANGAZA UTALII UBELGIJI,FLAVIANA MATATA ATEULIWA

...
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, amebainisha kwamba ili kukuza utalii tayari ameanza mazungumzo na klabu ya KRC Genk anakocheza mtanzania Mbwana Ally Samatta ili kuweza kutangaza utalii nchini Ubelgiji.

Waziri Kigwangalla amesema kwamba wakati huu wapo kwenye kuandaa mkakati mahsusi, kwa ajili ya kujitangaza kwenye nchi hiyo.

"Tayari pia tumeanza mazungumzo na mcheza soka wa kulipwa, Ndg. Mbwana Samatta, ili tutumie jina lake kufungua soko jipya la Utalii nchini Belgium. Tunaandaa mkakati mahsusi kwa ajili ya kujitangaza kwenye nchi hii"!

Mbali na kuweka mipango juu ya Samatta, Waziri huyo amemuomba Mwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata kukubali uteuzi wake wa kuwa balozi wa hiari wa Utalii nchini.

"Tunakushukuru na kukupongeza Ndg. Flaviana Matata kwa uzalendo wako. Tutakupa hati ya shukrani na pia tunakupa Safari ya siku 5 kwenye maeneo ya vivutio siku yoyote utakayokuwa tayari. Pia tutaomba ukubali uteuzi wangu wa kuwa Balozi wa hiari wa utalii"

Pamoja na hayo Waziri amesema kwamba tayari amekwisha kamilisha kazi ya kubuni kauli mbiu ya #TanzaniaUnforgettable ambayo itaitambulisha nchi kwenye masoko ya utalii.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger