Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amewakabidhi wafanyabiashara wadogo Vitambulisho Maalumu vilivyotolewa na Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli huku akiwataka kuwa waaminifu na wazalendo wa taifa lao
Uzinduzi wa kutolewa vitambulisho hivyo umefanyika Alhamisi Januari 10,2019 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la halmashauri ya wilaya ya Shinyanga .
Akizindua zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amewataka Wafanyabiashara hao kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha zinazopatikana kutokana na shughuli wanazofanya ili ziweze kuwanufaisha,na kuwaondoa katika hali ya Umasikini.
“Tuwe na nidhamu ya matumizi ya fedha , umeshalipa kodi yako ya shilingi 20000 kwa mwaka mmoja utapewa kitambulisho na mwaka mwingine unatakiwa ulipe, sasa utakapolipa maana yake fedha utakazokuwa unaendesha biashara zisiingie tumboni tu zikafanye pia maendeleo kwenye familia yako” alisema Mboneko
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi ametahadharisha Wafanyabiashara wakubwa kutojihusisha na udanganyifu kuuza bidhaa zao kwa kuwatumia wafanyabiashara ndogondogo wenye vitambulisho vilivyotolewa na Mheshimiwa Rais kwani kwa kufanya hivyo ni kukwepa ulipaji wa kodi
“Unakuta mtu anaduka anatoa bidhaa za kwake anawapatia hawa wafanyabiashara ndogondogo ambao hawalipi kodi kwa hiyo anafunga duka lake wakati bidhaa zake zikiendelea kuuzwa mtaani, huyu anakwepa kulipa kodi na tumeshawabaini na tutawachukulia hatua” alisema Mwangulumbi.
Kwa upande wao Wafanyabiashara ndogo ndogo wameshukuru na kupongeza hatua ya Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli kutoa vitambulisho hivyo ambavyo vitawasaidia kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu ikilinganishwa na hapo Mwanzo ambapo walikuwa wakipata usumbufu.
ANGALIA PICHA
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amewakabidhi wafanyabiashara wadogo Vitambulisho Maalumu vilivyotolewa na Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli huku akiwataka wafanyabishara kuwa waaminifu na wazalendo wa taifa lao . Picha zote na Steve Kanyefu Malunde1 blog

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua baadhi ya fomu ambazo mfanyabiasha ndogondogo anatakiwa kujaza taarifa zake ili apatiwe kitambulisho
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiongoza zoezi la kuwapatia vitambulisho baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria katika uzinduzi wa utolewaji wa vitambulisho uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akisisitiza jambo ambapo amewataka wafanyabishara kuzingatia usafi katika mazingira ya biashara zao.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (katikati),kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi na kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga Jumbe Samson wakisikiliza kwa makini baadhi ya maoni ya Wafanyabishara .
Mkuu wa Wilaya akisisitiza jambo kwa baadhi ya wafanyabishara waliohudhuria katika uzuinduzi wa kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara ndogondogo
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Jumbe Samson akiwasisitiza wafanyabishara kutumia vyema vitambulisho hivyo ili kuepuka usumbufu pindi ukaguzi wa kuwabaini wasio na vitambulisho utakapoanza.
Baadhi ya Wafanyabishara wakiwa ukumbini
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiongoza zoezi la kuwapatia vitambulisho baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria katika uzinduzi wa utolewaji wa vitambulisho uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (katikati),kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi na kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga Jumbe Samson wakisikiliza kwa makini baadhi ya maoni ya Wafanyabishara .
Mkuu wa Wilaya akisisitiza jambo kwa baadhi ya wafanyabishara waliohudhuria katika uzuinduzi wa kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara ndogondogo
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Jumbe Samson akiwasisitiza wafanyabishara kutumia vyema vitambulisho hivyo ili kuepuka usumbufu pindi ukaguzi wa kuwabaini wasio na vitambulisho utakapoanza.
Baadhi ya Wafanyabishara wakiwa ukumbini
0 comments:
Post a Comment