Friday, 4 January 2019

NECTA YAFUTA MATOKEO YA WANAFUNZI WALIOANDIKA MATUSI KWENYE MITIHANI...ANGALIA MATOKEO HAPA

...
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) leo Ijumaa Januari 4, 2019 limetangaza matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 2018, kueleza kuwa ufaulu umeongezeka ikilinganishwa na matokeo ya 2017.

Hata hivyo matukio ya wanafunzi kuandika matusi limeendelea  kujitokeza ambapo  Baraza la mitihani Tanzania limeyafuta matokeo yote ya watahiniwa tisa wa kidato cha pili walioandika matusi kwenye script zao katika na tumeelekeza bodi za shule kuwachukulia hatua za kinidhamu ili kukomesha tabia hii ya wanafunzi.

Akizungumza leo mjini Dodoma katibu mtendaji wa baraza hilo, Dk, Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa 1,302,461 wa darasa la nne waliofanya mtihani huo sawa na asilimia 95.58, waliofaulu kwa kupata daraja A, B, C, na D ni 1,213,132 sawa na asilimia 93.16.

Hata hivyo wanafunzi 89,093 sawa na asilimia 6.84 wamepata alama za daraja E ambalo ni ufaulu usioridhisha.

“151 walishindwa kufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa na utoro,” amesema.

Dk Msonde amesema mwaka 2018 takwimu za matokeo zinaonyesha kuwa ufaulu wa watahiniwa kwa masomo yote uko juu ya wastani.


“Ubora wa ufaulu umezidi kuimarika kwa kuwa watahiniwa waliofaulu kwa daraja A, B na C umeongezeka kwa asilimia 0.03 ikilinganishwa na mwaka 2017,”amesema Dk Msonde.

Kuhusu kidato cha pili, Dk Msonde amesema watahiniwa 506,235 walisajiliwa kufanya mtihani huo sawa na asilimia 92.87, kwamba wanafunzi 38,842 sawa na asilimia 7.13 hawakufanya mtihani kutokana na ugonjwa na utoro.

Amesema wanafunzi 452,273 sawa na asilimia 89.68 wamepata alama za ufaulu zitakazowawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

Amesema wanafunzi 52,073 sawa na asilimia 10.32 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

Amesema mwaka 2017 wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 89.32 walipata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu, kwamba ikilinganishwa na 2018, ufaulu wa mwaka jana umeongezeka kwa asilimia 0.36.

Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa ya Kidato cha Pili (FTNA) 2018 Na Darasa la nne (SFNA) 2018 yametangazwa..Yaangalie hapa na pia mpangilio wa ufaulu ngazi ya mikoa na halmashauri

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger