Sunday, 20 January 2019

MWANAUME ALIYEMUUA MKEWE NA WAKILI WAKE NAYE AJIUA

...
Mwanamume aliyeshtakiwa kwa kumuua mke wake miaka kadhaa iliyopita nchini Uhispania sasa anadaiwa kumuua wakili wake na kisha naye kujiua.

Jose Javier Salvador Calvo, 50, aliruka kutoka kwenye daraja la mji wa mashariki wa Teruel polisi walipojaribu kumkamata.

Kisa hicho kimewagutusha watu nchini Uhispania na kuzua mjadala mkali kuhusu sheria ya mzozo wa kinyumbani nchini humo.

Akizungumzia vifo hivyo waziri mkuu wa Uhispania, Pedro Sánchez ameapa kuendeleza juhudi za kukabiliana na visa vya unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Ikumbukwe kwamba Jose Javier Salvador Calvo alimpiga risasi na kumuua mke wake, Patricia Maurel Conte, 29, mwezi Mei mwaka 2003 katika eneo la Aragon kaskazini mashariki mwa Uhispani.

Baada ya kuachilia chini ya sheria maalum mwaka 2017, muuaji huyo alijiingiza katika uhusiano wa kimapenzi na Rebeca Santamalia Cáncer, 47,wakili aliyemtetea mahakamani aliposhtakiwa kwa mauaji,kwa kujibu wa vyombo vya habari vya Uhispania.

Polisi ilimpata wakili huyoakiwa ameuawa kwa kudungwa kisu katika nyumba ya Salvador Calvo iliyopo eneo la Aragon siku ya ijumaa baada ya mume wake kupiga ripoti kuwa ametoweka.

Muda mfupi kabla ya saa sita usiku mwili wa mshukiwa aliyejirusha kutoka daraja la Teruel, mji uliyopo kilo mita 150 kutoka eneo la tukio, ulipatikana na polisi waliyokuwa kazini.

Mwakilishi wa mamlaka ya mtaa huo Carmen Sánchez amewaambia wanahabari kuwa wakili huyo alikua mhasiriwa wa "unyanyasaji wa kijinsia".
Chanzo : Bbc
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger