Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Katavi, inawashikilia askari mgambo wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani hapa, kwa tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa ya magunia matatu ya mkaa pamoja na Sh 20,000.
Wawili hao wanadaiwa kupokea rushwa hiyo kutoka kwa wananachi ili waweze kusafirisha mkaa bila kuwa na leseni wala kibali cha mamlaka husika.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi, Christopher Nakuwa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Lazaro Kambaulaya na Charles Kisauko.
Nakuwa alikuwa akitoa taarifa ya utekelezaji ya majukumu ya Takukuru mbele ya waandishi wa habari jana mjini hapa kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2018.
Katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba mwaka jana Takukuru iliendelea kutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rukwa namba 11 ya mwaka 2007.
Kipindi hicho taasisis hiyo imepokea malalamiko 18 ya vitendo vya rushwa na kufungua majalada matano ikiwemo ya migogoro ya viwanja.
Peti Siyame - Habarileo Mpanda
0 comments:
Post a Comment