Na, Naomi Milton Serengeti Jummane Azori(43) mkazi wa Songambele Kigoma na Pala Yoram(29) mkazi wa Uvinza Kigoma wamehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kila mmoja katika kesi mbili tofauti moja ni kuhujumu uchumi na ya pili ni kupatikana na silaha ambayo ni Bunduki aina ya SMG. Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile katika mahakama ya wilaya ya Serengeti baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa kwa upande wa mashtaka dhidi ya washtakiwa hao. Kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo mwendesha mashtaka wa Jamhuri Emmanuel…
0 comments:
Post a Comment