Mchezo kati ya Simba na Bandari FC
Baada ya Simba kutolewa na Bandari FC katika nusu fainali ya michuano ya SportPesa jioni ya leo, Afisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara ameonesha waziwazi kusikitishwa na matokeo hayo.
Simba imeambulia kichapo cha mabao 2-1 katika uwanja wa taifa baada ya kutangulia bao moja katika kipindi cha kwanza lililofungwa na Meddie Kagere katika dakika ya 45, huku mabao yote ya Bandari FC yakifungwa katika kipindi cha pili kupitia kwa William Wadri dakika ya 59 na Wilberforce Lugogo katika dakika ya 72.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Afisa Habari huyo, ameandika akionesha kusikitishwa na matokeo hayo huku akiwatakia pole mashabiki wa klabu hiyo.
"Togwa limeingia nzi!!. Ukisikia kuharibiana siku ndio huku Okey poleni Wanasimba wote #SportPesaCup2019", ameandika Manara.
Kwa matokeo hayo sasa Simba inasubiri kucheza mchezo wa mshindi wa tatu na timu itakayofungwa mchezo mwingine dhidi ya Mbao FC na Kariobang Sharks.
0 comments:
Post a Comment