Thursday, 24 January 2019

MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU KUHUSU OLIVER MUTUKUDZI

...
Kama umeshawahi kuiona filamu ya Neria, basi bila shaka utakuwa unaujua wimbo wa Neria ambao umeimbwa kwa sauti nzuri nzito, ambayo hautachoka kusikia masikioni mwako, huku vinanda vyake vikiusuuza moyo wako na utamu wake masikioni mwako.

Oliver Mutukudzi aliimba wimbo huo akiwa na lengo la kumliwaza dada yake Neria aliyefiwa na mumewe na kukumbana na manyanyaso ya wakwe zake.

Mutukudzi alizaliwa September 22, 1952 nchini Zimbabwe katika eneo la Highfield, ambako ni Uswahilini haswa ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo Harare.

Kutokana na sauti yake nzuri na ya kuvutia anapoimba aliyojaliwa na Mungu. Oliver aliingia kwenye muziki na kuwavutia wengi tangu miaka ya 77, umauti umemfika akiwa na albam 59 alizozifanya, na kujiwekea heshima kubwa duniani.

Haya ni mambo muhimu ambayo unapaswa kuyajua kuhusu Oliver Mutukudzi.

1. Ni baba wa watoto watano, watoto wake wawili ni wanamuziki wakubwa nchini Zimbabwe, lakini kwa bahati mbaya mmoja, Sma Mutukudzi alifariki dunia mwaka 2014 kwa ajali ya gari.

2. Ana albam 59 mpaka anakutwa na umauti Januri 23, 2019.

3. Ameshajizolea tuzo zaidi ya 20 za kitaifa na Kimataifa

4. ameshawahi kuwa katika ukurasa wa mbele wa Gazeti kubwa la Marekani la Time, na kuwa msanii pekee kutoka Zimbabwe kufanya hivyo.

5. Alikuwa muigizaji wa filamu, ikiwemo filamu ya Neria ambayo ilizidi kumpa umaarufu Afrika na duniani.

6. Mwaka 2011, jarida la Forbes lilimtaja kuwa miongoni mwa watu maarufu 40 wa Afrika wenye nguvu, akiwemo muandishi wa vitabu Chinua Achebe na msanii wa muziki Akon.

7. Mutukudzi amefariki tarehe moja na rafiki yake kipenzi, msanii wa muziki wa Afrika Kusini, Hugh Masekela, ambaye alifariki Januari 23, 2018.

8. Ameshawahi kufanya kazi na msanii wetu wa hapa nyumbani Lady Jaydee, na hata kumleta kuja kufanya naye show katika moja ya kumbi Jijini Dar es salaam.

9. Ameshawahi kupewa degree ya heshima kutokana na kuwa philanthropist

10. Amefanya kazi na bendi kubwa nchini Afrika Kusini ambayo inahusisha wanaume watupu, ya Ladysmith Black Mambazo, ambao kwa pamoja waliurudia wimbo wa Neria na kutoa nyinginezo

Kifo cha Oliver Mutukudzi kimeacha pengo kubwa katika nchi ya Zimbabwe, kwani Mutukudzi hakujulikana kama msanii tu, bali alikuwa na heshima kubwa aliopewa wana Zimbabwe, kutokana na matendo yake na roho yake ya upendo ya kusaidia watu.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger