Friday, 11 January 2019

MAKONDA "MNIOMBEE,NIKIKUA NIWE KAMA RAIS MAGUFULI"

...

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewaomba viongozi wa dini wamuombee ili atimize ndoto ya kuwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Muda mfupi uliopita akizungumza katika mapokezi ya ndege aina ya Airbus A220-300 uwanja wa ndege, Makonda amewataka viongozi wa Dini kumuombea juu ya ndoto yake ya kuwa kama Rais Magufuli kwa kuwa ni mtu wa kutekeleza.

"Viongozi wa dini naomba mniombee, nataka nikikua niwe kama Rais Magufuli, haya ni maombi yangu kabisa, kwa sababu ni mtu wa kutekeleza, usiyeyumbishwa,umehakiksha Mungu kwanza na unaipenda Tanzania kuliko hata familia yako"- Paul Makonda.

Makonda ameongeza, "hivi ulivyo Rais wetu angekuwa mwingine Watoto wake tungekuwa tunagombana nao mtaani lakini Wewe umehakikisha hakuna anayeingilia jukumu lako kama Baba wa familia" Makonda

Pamoja na hayo Makonda amemwambia Rais Magufuli, yeye na wakazi wa Dar es salaam wamekwenda kumuunga mkono kwa kuwa alitoa ahadi kutoka kwenye ilani ya CCM na anatekeleza ikiwemo elimu bure

"Nilipotoa tangazo la kuja hapa nilisema waje wale waliowahi kutoa ahadi na wakatekeleza" Makonda.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger