Saturday, 12 January 2019

MAGUFULI : KUMBE MIMI NAFUU KULIKO DKT. BASHIRU,HOTUBA ZAKE ZINASHANGAZA

...
Rais John Magufuli ameweka wazi kuwa hotuba za Katibu mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally huwa zinamshangaza kwa namna ambavyo anazitoa bila uoga jambo ambalo humfanya yeye ajione ni mpole.


Mwenyekiti huyo wa CCM alieleza hilo jana kwenye hotuba yake wakati wa mapokezi ya ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 iliyowasili nchini jana mchana Januari 11, 2019 kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

''Dkt. Bashiru amekuwa muwazi, huwa namuangalia kwenye hotuba zake saa nyingine nasema kumbe mimi nafuu bwana kuliko huyu jamaa'', alisema.

Rais alieleza kuwa Katibu wake huyo amekuwa akikemea ufisadi ambao ulikuwa ukishamili siku hadi siku lakini sasa yeye anapingana nao hadharani bila kujali.

Magufuli amewataka viongozi wote wa chama na Serikali kuendelea kuwatumikia wananchi kwa moyo mmoja ili kusaidia maendeleo na siku moja Tanzania itakuwa kama Ulaya.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger