Saturday, 26 January 2019

KIKWETE : VIONGOZI WA SERIKALI NI CHANZO CHA WAKIMBIZI

...

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema sababu zinazo sababisha ongezeko la wakimbizi duniani ni pamoja na viongozi wa serikali wa nchi husika.

Dkt. Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na umoja wa Mataifa ambapo ameeleza kwamba mwaka 2018 idadi ya wakimbizi ilifika milioni 68.5 ambapo idadi hiyo ndio kubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Rais Kikwete amesema kwamba baada ya vita kuu ya pili hii ndio idadi kubwa ya watu waliohama maeneo yao, wengine wakatoka nje ya nchi lakini wengine wakaishi ndani ya nchi lakini sio kwenye maeneo yale ambayo yalikuwa ni makazi yao.

"Kuna watu ndani ya nchi zao, viongozi ama wa serikali au wakati mwingine ni wa jamii, kwa sababu watu wanakimbia mateso, wakati mwingine ni uongozi, unakuwa na serikali ambayo ni katili lakini wengine ni sera za kibaguzi ndani ya nchi ambazo zinawabagua watu kama ilivyo Myanmar, wanawakana wale wenzao ambao wanateswa kwa misingi ya dini, makabila kwa hiyo hayo ndio miongoni mwa mazingira ambayo sio tatizo la kubuni, ni tatizo dhahiri" .

Hata hivyo mapema wiki hii, Baraza la wakimbizi duniani, WRC limetoa wito kufanyike mabadiliko katika mifumo ya suala la wakimbizi duniani kwa ajili ya kulinda maslahi ya watu waliolazimika kukimbia ikiwemo walio wakimbizi wa ndani na jamii zinazowahifadhi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger