Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amepiga marufuku tabia ya Maafisa Uhamiaji kuwatambua wahamiaji haramu kwa kigezo cha Pua ndefu.
Lugola amepiga marufuku hiyo jana alipokuwa akiongea kwenye moja ya mikutano yake mkoani Kagera ambako yupo kwenye ziara ya kikazi aliyoianza Januari 2, mwaka huu.
''Idara ya uhamiaji kutambua wahamiaji haramu kwa kigezo cha pua ndefu, kuimba wimbo wa taifa na urefu wa mwili wake nimepiga marufuku'', amesema.
Aidha Lugola ameongeza kuwa Idara ya Uhamiaji ina taratibu na vigezo vyake vya kiweledi katika kushughulika na suala hilo hivyo amesisitiza viendelee kutumika kubaini nani raia na nani sio raia.
0 comments:
Post a Comment