Wafanyakazi wa kampuni ya Beijing New Building Material (BNBM) inayotengeneza vifaa vya ujenzi, wameilalamikia kampuni hiyo kwa kushindwa kuwalipa stahiki zao pale wanapoachishwa kazi. Wakizungumza na Darmpya wafanyakazi hao walisema kuwa kampuni hiyo imekuwa na tabia ya kuwaachisha kazi wafanyakazi wake bila kuwapa malipo yao wanayostahili hasa wale wanaoonekana kutetea haki zao. Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi katika kampuni hiyo Ramadhani Shukuru amesema “Wafanyakazi wengi wamefukuzwa kazi na wana mikataba lakini stahiki zao hawakuzipata, malalamiko haya tumeshayapeleka hadi ngazi ya wilaya wakasema watafuatilia lakini mpaka muda huu hatujawaona”. Ameongeza kwa…
0 comments:
Post a Comment