Miaka ya 2000 kurudi nyuma walikuwepo watu maarufu sana katika maeneo mengi ya usukumani, Waleta Mvua wa Asili (BAGHEMI BHA MBULA), mvua zikigoma kama sasa walikuwa wakitafutwa kwa gharama yoyote ile.
Basi kijiji kinajadili kupitia mkutano wake (Dagashida), ulioongozwa na Ntemi, Mganga anafuatwa anafanya matambiko yake, kuna wakati mvua ilinyesha kwa kuamini wamefanikiwa maombi yao, kuna wakati iligoma na kuona mganga kashindwa kazi..
Yalikuwepo pia maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya kaudhimisha tambiko hilo la kimila ambayo yalikuwa ni visima, milima na maeneo mengine muhimu kwa kazi hiyo.
Yalikuwepo pia maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya kaudhimisha tambiko hilo la kimila ambayo yalikuwa ni visima, milima na maeneo mengine muhimu kwa kazi hiyo.
Walikuwepo wazee maalumu kwa kazi hiyo (Wanaume kwa wanawake) ambao walikuwa na mavazi yao rasmi yenye rangi ya nyeusi na nyekundu.
Siku ya matambiko walichinja ng'ombe mweusi, huko milimani/visimani, wanampika kwenye chungu bila kumwekea chumvi na kutafunwa bila ugali au wali, tena wanapakulia kwenye majani.
Mtaalamu huyo alikuwa akilipwa ujira wa Ng'ombe mmoja, pia wakati akitekeleza shuguli hizo alikuwa akitunzwa sana kwa sababu alionekana kuleta neema katika eneo hilo.
Lakini pia ilikuwepo siku maalum ya kuadhimisha siku hiyo ya matambiko kwenda kuabudu (KUHUMBA), pia kama watabaini kuna mtu (ke/me) anazuia hayo maombi yao yasifanikiwe walikuwa wakilowekwa kwenye dimbwi la maji na kuchapwa fimbo, pia kufukuzwa kijijini.
........HAWA JAMAA WALISHAPOTELEA WAPI.........
0 comments:
Post a Comment