Dogo Janja akiwa na mwanamke anayedaiwa kuwa mpenzi wake mpya
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abdulaziz Chende maarufu 'Dogo Janja' ameonekana akiwa kwenye mapozi yenye utata na mwanamke ambaye anadaiwa kuwa ndiye mrithi wa Irene Uwoya.
Picha pamoja na video zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha Janjaro akiwa na mwanamke asiyefahamika jina na wengi kudai kuwa Irene Uwoya amepinduliwa kwa Dogo Janja, ikiwa mpaka sasa wawili hao hawajaweka wazi kuachana.
Uwoya na Dogo Janja walianza kurushiana maneno ya mafumbo katika mtandao wa Instagram Januari 07, hali ambayo ilitafsiriwa kuwa ni wazi kuwa ndoa yao itakuwa imevunjika.
Baada ya sakata hilo, baba mlezi wa Dogo Janja, Madee Ali 'Seneda' ameingilia kati suala hilo na kuwaonya kutorushiana maneno mitandaoni.
0 comments:
Post a Comment