Friday, 18 January 2019

DC KISHAPU ASIMULIA JINSI ALIVYONUSURIKA KIFO WAKATI WAKUJIFUNGUA

...
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba ameeleza changamoto za uzazi alizopitia wakati akitoa shuhuda kwenye kikao cha wadau wa afya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya JIONGEZE TUWAVUSHE, na kusema yeye ni miongoni mwa wanawake waliopitia adha hizo kwani alikuwa akijifungua watoto wakubwa mwenye uzito wa kilo tano. 

Talaba amesema alinusurika kupoteza maisha kwasababu ya huduma bora ya afya aliyopatiwa kutoka kwa wataalamu wa afya. 

“Mimi nimepitia matatizo ya uzazi kwasababu nilikuwa najifungua watoto wakubwa wenye kilo tano,kwa hiyo haikuwa kazi ndogo pengine nisinge zalia hospitali nzuri ningepoteza maisha,” alisema Talaba. 

Mkuu huyo wa wilaya ya Kishapu alisema jukumu la kuzuia vifo kwa watoto wachanga na kinamama wajawazito linagusa sekta zote, kwasababu ya changamoto mbalimbali zinazotajwa kusababisha vifo hivo ikiwemo ya ukosefu na upungufu wa miundombinu ya huduma za afya katika vituo vya afya. 

“Ni wajibu wa kila mwanajamii kusimamia nafasi yake katika kuokoa maisha ya mama na mtoto kwa kuhakikisha anatatua changamoto za kimiundombinu, na kutoa elimu sahihi ya sehemu husika ya kupata huduma bora za afya,” aliongeza Talaba. 

Mkoa wa Shinyanga leo januari 18,2019 umezindua kampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kwa jina la JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA yenye lengo la kuzuia na kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.

Na Malaki Philipo - Malunde1 blog
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger