Monday 21 January 2019

BODI YA DAWASA YAJIPANGA KUONGEZA MIRADI YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA

...
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akionyeshwa eneo linaloanzia mradi wa Bonyokwa utakaohudumia wananchi kuanzia Kimara mwisho hadi Bonyokwa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo juu ya mradi wa maji Kisukuru jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akiongea na wananchi eneo la Tabata Bonyokwa mara baada ya kufika kujionea maendeleo ya miradi ya maji.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Mhandisi Charles Makoye akimuelezea Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mradi mzima wa Kuchakata majitaka uliopo Toangoma leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.


Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na  na wajumbe wa bodi wa Mamlaka hiyo juu ya mradi wa Kuchakata majitaka Toangoma Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Mhandisi Charles Makoye akimuonyesha Mkurugenzi wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na wajumbe wa bodi wa Mamlaka hiyo moja ya Chemba inayohifadhi majitaka katika mradi wa Kuchakata majitaka Toangoma leo Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Mhandisi Charles Makoye akimuelezea Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange juu ya mradi mzima wa Kuchakata majitaka uliopo Toangoma leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza na wajumbe wa bodi wa Mamlaka hiyo mara baada ya kufanya ziara katika mradi wa Kuchakata majitaka Toangoma leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akiwa na wajumbe wa bodi wakiendelea na ziara.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Mhandisi Charles Makoye akitoa maelezo machache juu ya mradi wa maji Kiwica- Mbagala Kijichi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akitoa majumuisho juu ya ziara yao ya siku tatu waliyofanya katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wamehitimisha ziara yao ya siku tatu kwa kutembelea miradi mbalimbali inayosimamiwa na Mamlaka hiyo.

Ziara hiyo ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani imemalizika kwa Mwenyekiti wa bodi Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange kutoa tathmini ya jumla ya mambo waliyojifunza.

Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara hiyo, Jenerali Mstaafu Mwamunyange amesema wananchi wana matarajio makubwa na DAWASA ya kupata huduma ya majisafi inayoaminika.

Jenerali Mstaafu Mwamunyange amesema kwenye ziara ya siku tatu wamejifunza mengi na wameona ni namna gani DAWASA wanafanya jitihada kubwa kuhakikisha wanafikisha maji kwa wananchi wote ili kufikia malengo ya serikali.

Amesema kuwa, pamoja na yote kuna changamoto zinazoikabili DAWASA ikiwa ni pamoja na kupasuka kwa mabomba kutokana na miundo mbinu chakavu na kupelekea kupotea kwa maji mengi na watu wanaojiunganishia maji kiholela kitu kinachopelekea Mamlaka kupoteza fedha nyingi sana.

Ameeleza kuwa Changamoto nyingine ni majitaka na hilo linasababishwa na kuwa na maeneo machache yaliyokaribu na wananchi yanayopokea maji hayo na DAWASA wanaendelea kufanya jitihada za kujenga miundo mbinu itakayokuwa rafiki ikiwemo na kuleta magari yao yatakayokuwa yanachukua majitaka kwa bei nafuu.

“Mradi wa kuchakata majitaka ni jambo la msingi sana na utakuwa na faida kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo jirani ila bado una changamoto kwani maji yanayozalishwa na kupelekwa kwa wananchi ni mengi tofauti na yale yanayoenda kuchukuliwa,” amesema Jenerali Mstaafu Mwamunyange.

Kwa upande wa Mjumbe wa Bodi wa DAWASA Mhandisi Gaudence Aksante amesema kuwa, lazima kuweka mkakati wa kupunguza upotevu wa maji ili mamlaka kuongeza kipato na maji hayo yamekuwa yanapotea kutokana na mtandao wa zamani kuwa mdogo na kwa sasa maji ni mengi sana.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja amepokea ushauri huo kutoka kwa bodi ya wakurugenzi ikiongozwa na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na watajitahidi kuhakikisha wanapanua mtandao wa maji ili kupunguza upotevu wa maji.

Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi ilitembelea miradi ya ndani ya Dar es Salaam na ile ya Mkoa wa Pwani ikiwemo mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Juu na Ruvu Chini, Ujenzi wa matanki Bagamoyo, Changanyikeni, Kibamba, Kisarawe, maunganisho mapya ya wateja Salasala, mradi wa uchakataji majitaka Toangoma na mradi wa maji Kijichi, Kiwalani, Bonyokwa na maeneo mengine ya Jijini Dar es Saalam.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger