Friday, 18 January 2019

ANUSURIKA KUPOFUKA BAADA YA KUBUGIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME 'VIAGRA'

...

Mtu ambaye aliripotiwa kuwa alikunywa chupa 30 zenye ujazo wa mililita za dawa aina ya sildenafil, ambayo hutumiwa kusisimua sehemu za siri za kiume, alijikuta akipoteza uwezo wa kuona, ambao ni pamoja na kudhoofisha uwezo wa kuona usiku, kwa mujibu wa jarida la utafiti wa afya lililochapishwa hivi karibuni.


Mtu huyo, ambaye hakutajwa na anasemekana kuwa na umri wa zaidi ya miaka hamsini, alikunywa mara kumi zaidi ya kiwango kinachoshauriwa, IFLScience ilisema.

Baadaye mtu huyo alikwenda kwa madaktari wa macho wa macho wa kituo cha Massachusetts Eye and Ear Infirmary jijini Boston ambako alieleza kuwa alikuwa na tatizo la kuona usiku na alikuwa akiona vitu vye umbile la donati, kwa mujibu wa jarida hilo la IFLScience.

Madaktari walisema baada ya kutafiti dalili zote — isipokuwa ya kuona vitu vyenye umbile la donati— hali yake ilikuwa nzuri baada ya kupata matibabu. Walisema alipata tatizo katika retina (sehemu inayopokea nuru) za macho yake, jari hilo lilisema.

Dawa hiyo ya Sildenafil hufanya kazi kwa kuongeza kasi ya mwenendo wa damu kuelekea sehemu za siri za mwanamume, na kumuwezesha mtu aliye na tatizo la sehemu hizo kutofanya kazi, kuweza kujamiiana.

Katika shauri la mtu huyo, hata hivyo, kiwango cha sildenafil alichokunywa kinaweza kuwa kilisababisha “mishipa ya damu ya macho kutanuka kwa haraka au kwa nguvu, na kusababisha uharibifu,” limeripoti jarida hiyo la IFLScience.

Lilisema hata kutumia kiwango kinachoshauriwa cha cha sildenafil kunaweza kusababisha tatizo la kuona, Jamie Alan, profesa msaidizi wa masuala ya dawa na sumu wa Chuo Kikuu cha Michigan aliiambia Yahoo.

Hata tovuti ya Viagra imeonya kuwa “kupotea ghafla kwa uwezo wa kuona wa jicho moja au yote" ni moja ya madhara yanayoweza kusababishwa na dawa hiyo.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger