Monday, 7 January 2019

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA ARUDI KWA KASI YA AJABU..AFUNGUKA MBELE YA BASHIRU

...
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa ameanza kuitumikia CCM kwa ari mpya na nguvu mpya ili kukiimarisha chama hicho. 

Kwilasa ambaye hivi karibuni alirudishiwa uanachama baada ya kusimamishwa uanachama wa CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)akiwa mwenyekiti mkoa wa Shinyanga akidaiwa kukiuka misingi ya Katiba ya chama hicho mwaka 2017 ,amesema yupo tayari kutumwa kufanya jambo lolote kwa maslahi ya CCM. 

Kwilasa ameyasema hayo leo Jumatatu Januari 7,2018 wakati Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na Watendaji wa CCM ngazi ya kata,wilaya na mkoa kwenye Ukumbi wa CCM Shinyanga. 

“Ninawaomba kwa jambo lolote nitumieni na nitatumika kwa maslahi Chama na ninaahidi kwamba tutafanya kazi pamoja na wanachama ili kuleta maendelo ya mkoani Shinyanga”,alisema Kwilasa huku akishangiliwa na wafuasi wa CCM ukumbini. 

“Ninawaombea kwa mwenyezi awape afya njema ili muweze kuchapa kazi na kujenga chama chetu na mimi mbele yenu ninaahidi nitakuwa mwanachama mwaminifu na mwadilifu kwa maslahi ya chama chetu na kukijenga chama na kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama chetu”,aliongeza. 

“Nawashukuru sana mwenyekiti wa CCM taifa Dkt. John Pombe Magufuli na katibu mkuu Dkt. Bashiru Ally kwa usimamizi wa chama chetu,chama hiki kimeonekana kuwalenga zaidi wanyonge kwani haki zinatendeka hakuna jambo lolote la uonevu linaweza kupita mbele yenu mkaliangalia tu”,alisema Kwilasa. 

Miongoni mwa wenyeviti wa mikoa ambao Machi, 2017 walifukuzwa uanachama kwa kudaiwa kukiuka katiba ya CCM ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu, Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Erasto Kwilasa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara, Christopher Sanya.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Erasto Kwilasa akishikana mkono na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally leo Januari 7,2019 katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na Watendaji wa CCM ngazi ya kata,wilaya na mkoa kwenye ukumbi wa CCM Shinyanga. 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Erasto Kwilasa akizungumza baada ya kukaribishwa atoe neno na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally
Erasto Kwilasa akizungumza na kuahidi kuwa mwanachama mwaminifu na mwadilifu wa CCM.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger