Hali ya simanzi na huzuni imegubika familia ya msanii wa bongo Fleva Ali Kiba baada ya babake kufariki dunia mapema leo.
Mzee Saleh Kiba alifariki katika hospitali ya Muhimbili ambapo alikuwa amelazwa.
Kulingana taarifa za mdogo wa mwanamuziki huyo ambaye pia ni msanii Abdu Kiba alithibitisha habari hizo.
Msanii huyo amesema kuwa msiba unafanyika katika mtaa wa Kariakoo eneo la Muheza ambapo ndio nyumbani kwao.
Kulingana na afisa wa Uhisiano mwema katika hospitali ya Muhimbili Neema Mwangomo amesema kuwa Mzee Saleh alifikwa na mauti yake saa kumi na mbili alfajiri.
Aliongezea kuwa marehemu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo tangu tarehe 27 mwezi Disemba.
Chanzo:Bbc
0 comments:
Post a Comment