London, England. Manchester United na Barcelona zimeshindwa kutumia vizuri viwanja vyao vya nyumbani baada ya kulazimishwa sare 1-1 na Bayern Munich na Atletico Madrid katika michezo ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa jana.
Manchester United wakiwa kwenye uwanja wao wa Old
Trafford, walipata bao la kuongoza dakika 58, kupitia nahodha wake
Nemanja Vidic akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona, kabla ya Bastian
Schweinsteiger kuwasawazishia mabingwa watetezi Munich dakika 67,
akimalizia mpira wa kichwa kutoka kwa Mario Mandzukic.
Bayern walipata pigo dakika za mwishoni baada ya
kiungo wake Schweinsteiger kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya
Wayne Rooney.
Kwa mara ya nne mfululizo msimu huu mechi kati ya
Barcelona na Atletico Madrid inashindwa kutoa mshindi baada ya jana
kutoka sare 1-1 kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Neymar aliinusuru Barcelona na kipigo kwa kufunga
bao la kusawazisha dakika 71, baada ya Diego kuifungia Atletico goli la
kuongoza dakika 56.
Timu zitakazofuzu kwa nusu fainali zitajulikana wiki ijayo kwenye mechi za marudiano.
Leo kuna mechi nyingine mbili za robo fainali kati ya PSG dhidi ya Chelsea na Real Madrid wataonyeshana kazi na Dortmund.
Jose Mourinho ameitoa Chelsea katika mbio za
ubingwa, lakini anaamini vijana wake watathibitisha ubora wao leo dhidi
ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya
Mabingwa.
0 comments:
Post a Comment