Wanafunzi walioandaa mgomo wa jana Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) huenda wakakumbwa na hatua za kinidhamu kwa kosa la kukikuka sheria ndogo ya Chuo kwa kuandaa mkusanyiko pasipo kibali cha Menejimenti.
Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo taaluma Florens Luoga amesema kuwa hadi sasa
mamlaka za nidhamu chuoni hapo zinendelea na uchunguzi kubaini nani
alihusika na ni kwa namna gani na baada ya hapo hatua za kinidhmu
zitafuata.
“Taratibu
na sheria ndogo za chuo haziruhusua mtu kuandaa mkusanyiko ambao
haujaidhinishwa na menejimenti na kimsingi taratibu hizo lazima
ziheshimiwe ili kuzifanya kuendelea kuwa imara hivyo tunasubiri ripoti
ya walio husika endapo itaonesha kuwa wanamakosa basi watachukuliwa
hatua za kinmidhamu,” amesema Luoga.
0 comments:
Post a Comment