DIAMOND F/ P-SQUARE
Huu ni wimbo wa Diamond aliowashirikisha mapacha maarufu zaidi Afrika, Peter na Paul Okoye wa kundi la P-Square. Video ya wimbo huo ilifanyika April 24 nchini Afrika Kusini. Na sasa hitmaker huyo kupitia post yake ya Instagram amewaeleza mashabiki wake kuwa collabo hiyo inatoka ‘soon.’
Wimbo huo unatoka ikiwa ni takriban mwaka mmoja sasa kundi la P-Square halijaachia wimbo wake mpya. Wimbo rasmi wa mwisho wa kundi hilo la nchini Nigeria kutoka ulikuwa ni Collabo waliomshirikisha Don Jazzy. Miezi ya hivi karibuni wawili hao waliingia kwenye mgogoro wa kifamilia uliopelekea kuondolewa kwa kaka yao Jude kama meneja wao wa muda mrefu.
Mgogoro wa wawili hao ulipelekea kuwepo kwa kila dalili za kundi hilo kuwa limevunjika huku kila mmoja akianza kuwekeza nguvu zake kwenye miradi binafsi. Kwahiyo Diamond ana collabo kubwa mkononi mwake itakayoitikisa Afrika nzima huku kiu ya sauti za Peter na Paul wakiwa pamoja tena zikiifanya kuwa ‘collabo ya dhahabu.’
Kingine kwa watu waliobahatika kuiona video ya ngoma hiyo wanasema ni video kali itakayomweka Diamond level nyingine.
Na huenda staa huyo ameitengenezea timing nzuri zaidi ya kuiachia itakayoangukia kwenye msimu wa tuzo za BET mwishoni mwa mwezi huu. Kwa kuachia collabo kubwa kama hiyo katika msimu huo, anajitengenezea sababu ya kuwa msanii anayestahili kuishinda tuzo ya Best International Artist: Africa mwaka huu.
PAPA WEMBA F/ DIAMOND
Wiki tatu kabla mauti hayajamkuta Papa Wemba kwa kuanguka jukwaani na kufariki wakati akitumbuiza mjini Abidjan, Ivory Coast, April 24, muimbaji huyo mkongwe aliingia studio kurekodi wimbo na Diamond. Tarehe ambayo Papa Wemba alifariki, ndiyo ambayo Diamond alikuwa location kushoot video ya wimbo aliowashirikisha P-Square.
Kwahiyo ni bahati na heshima kubwa kwa staa huyo wa Tanzania kufanikiwa kushirikishwa na mwanamuziki huyo nguli aliyekuwa na sauti ya aina yake wiki chache kabla ya kifo chake.
Kupitia akaunti ya Instagram ya marehemu Papa Wemba ambayo bila shaka inaendelea kusimamiwa na watu wake wa karibu, imetangazwa kuwa wimbo huo utatoka June 24. Wimbo huo utakuwepo kwenye ile ambayo ingekuja kuwa album yake mpya, From Generation to Generation.
Kama zitatoka katika wiki zitakazofuatana, basi collabo hizi zitamfanya Diamond ateke vichwa vya habari vya Afrika na kumuongezea ukubwa wake unaoendelea kukua kila siku kwenye muziki wa Afrika.
0 comments:
Post a Comment