TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI,
DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) UNAORATIBIWA NA
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
Baraza linapenda kuwaarifu waombaji udahili wa kozi tajwa hapo juu na umma kwa ujumla kuwa, kwa sasa maombi yote yaliyowasilishwa mpaka tarehe 3 Juni 2016 saa sita usiku yameanza kuchambuliwa kwa ajili ya kuchagua waombaji wenye sifa stahiki. Zoezi la kuchambua waombaji udahili na hatimaye kuchagua waombaji wenye sifa stahiki na waombaji hao kuidhinishwa na mamlaka husika na kutangazwa litachukua muda wa wiki nne (4) kuanzia tarehe 3 Juni, 2016.
Baraza linatambua uwepo wa waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kuwasilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016. Waombaji wa namna hii na wengine wanaopanga kuwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) wanaombwa kuwa na subira mpaka hapo majina ya waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya kufungwa kwa mfumo watakapotangazwa.
Baada ya kutangazwa majina ya waombaji waliochaguliwa, Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) utafunguliwa tena kwa ajili ya kujaza nafasi za udahili ambazo zitakuwa hazijajazwa na waombaji waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi, 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016.
Baraza linatarajia kufungua tena Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kwa ajili ya kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada ya Kwanza wiki ya mwishoni mwa mwezi wa Sita, 2016.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 9 Juni, 2016
0 comments:
Post a Comment