Thursday 18 July 2019

Waziri Bitteko akerwa na Maafisa Madini wazembe wanaoikosesha serikali mapato kwa kutosimamia masoko ya Dhahabu

...
NA SALVATORY NTANDU
Serikali imewataka Watumishi wa Ofisi ya Madini ya Wilaya ya Kahama kijitathimini kama wanafaa katika nafasi zao za uongozi kutokana kuendelea kubainika kwa vitendo vya utoroshaji madini ya dhahabu vinavyofanywa na wachimbaji wadogo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Madini Dotto Bitteko baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika baadhi ya wanunuzi wa dhabubu (Brokers) katika eneo la kakola lilipo katika halmashauri ya Msalala na kubaini utoroshwaji wa madini.

Amesema ofisi yake imepata taarifa za kuwepo kwa wanunuzi 12 wanaonunua dhahabu katika eneo hilo bila yakuwa na vibali huku wengi wao wakiitorosha kwenda kuiuza katika nchi za Kenya na Uganda na kuikosesha serikali mapato huku maafisa wake wakika kimya.

Amesema katika ziara yake amebaini wizi huo mpya ambao maafisa wake hawajatoa taarifa za wafanyabiashara hao ambao wanaendelea kuihujumu nchi kwa kununua dhahabu katika masoko ambayo hayatambuliwi na serikali huku maafisa wake wakiwa hawatoai taarifa na kuchukua hatua.

Bitteko amesema kuwa wamembaini Mnunuzi ambaye amenunua   dhahabu kilo tatu yenye thamani ya shilingi Milioni 300 lakini mrahaba hakuweza kulipia hawezi kulipa kutokana na kununua kinyemela.

Amesema  Mnunuzi wa pili alinunua dhahabu kwa muda wa wiki mbili na alipata kilo 2.64 na kuuza kiasi cha shilingi Milioni 241 pia nae hakuweza kulipa mrahaba wa serikali.

Nae Kamishina wa Tume ya madini, Prof.Abdulkari Mruma amewataka wachimbaji mdogo kuhakikisha wanauza dhahabu zao kwenye masoko ili walipe kodi na wauze katika bei halali.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger