Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuru mkoa wa Dodoma imeingilia kati ujenzi wa mradi wa maji wa kijiji cha kelema kuu wilayani chemba baada ya kubaini thamani ya fedha iliyotumika kutoendana na kazi halisi na kuokoa shilingi Milioni 67 ,laki 5,42 elfu na mia 600.
Akitoa taarifa ya robo ya nne ya TAKUKURU kwa waandishi wa habari ya kuanzia Mwezi April hadi Juni 2019, mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Bw Sosthenes Kibwengo amesema kuwa hatua hiyo imefanyika ikiwa ni utekelezaji wa majukumu ya Takukuru chini ya kifungu cha saba [7] cha sheria ya kuzuia na kupamabana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 .
Mradi huo wa maji unagharimu kiasi cha Tsh.milioni 222,laki 9,elfu 78,mia 680 na ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2015.
“TAKUKURU mkoa wa Dodoma imeingilia kati mradi wa maji Kelema Juu,baada ya kubaini fedha iliyotumika kutoendana hali halisi na kazi iliyofanyika na uwekaji mabomba ukiwa chini ya kiwango hali iliyosababisha kutotoa maji na malipo yakiwa zidifu tofauti na makubaliano ya mradi na kuanzia tarehe 1,julai anaanza kurudia kuifanya kazi”
Aidha,Bw.Kibwengo amesema TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kuokoa na kurejesha serikalini Tsh.Milioni 11 laki 88,77elfu,mia 353 zilizolipwa bila utaratibu kama mshahara kwenye akaunti ya mwalimu aliyekuwa amefariki.
Katika hatua nyinyine bw Kibwengo amesema kuwa wamefanikiwa kumkamata Bw Gaston Meltus Francis amabaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Global Space East Africa Limited iliyopewa kazi ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Mima wilayani mpwapwa baada ya kubaini kampuni hiyo kulipwa isivyo halali kiasi cha shilingi milioni 86 laki nne na tano na mia mbili na tano kwa kazi ambazo hazikufanyika katika mradi huo.
Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoa, Bw Kibwengo ameongeza kuwa TAKUKURU imefanya uchambuzi wa mifumo mbali mbali ya utendaji na utoaji wa huduma ili kubaini m ianya na kushauri namna bora ya kuondokana nayo kwa lengo la kudhibiti vitendo vya rushwa huku pia ikitoa elimu kwa jamii juu ya rushwa na kuzindua vilabu 39 ngazi ya shule na vyuo katika mapambano dhidi ya rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Sanjari na hayo, TAKUKURU mkoa wa Dodoma imefuatilia na kukagua miradi 34 yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 32 milioni 545 laki nne na elfu kumi na nane mia moja na kumi na sita ambapo asilimia 95.4 ya matumizi ya fedha za miradi hiyo ikionekana kufanyika vizuri.
Hata hivyo ,TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imebaini viashiria vya jinai katika miradi minnne ambapo TAKUKURU inafanya uchunguzi uhalali wa malipo katika miradi hiyo kiasi cha Tsh.bilioni 1 ,milioni 409 na laki 9 yaliyofanyika katika miradi hiyo ambayo ipo katika sekta ya za ujenzi ,Afya,Elimu na Kilimo.
Katika taarifa ya TAKUKURU ya robo za Jauari,Machi hadi Juni Mwaka huu ,TAKUKURU mkoa wa Dodoma ilipokea taarifa135 za Rushwa na Makosa mengineyo katika michanguo ifuatayo ambapo,ardhi asilimia ,36%,serikali za Mitaa asilimia 31%,Polisi asilimia 8%,Kilimo asilimia 6%,mahakama na ujenzi kila moja asilimia 4%,asilimia 11% zilizobaki ni katika sekta za ,Afya,maji,Madini,Ukusanyaji mapato huku ikiendelea na Mashauri 30 mahakamani hadi sasa.
0 comments:
Post a Comment