Friday, 5 July 2019

Rais Magufuli kuzindua rasmi hifadhi mpya ya Taifa ya Burigi iliyoko Chato

...
Rais John  Magufuli anatarajiwa kuzindua rasmi Hifadhi ya Taifa ya Burigi huko Chato siku ya Jumanne Julai 9,  mwaka huu, ambayo imepandishwa hadhi hivi karibuni kutoka lililokuwa pori la akiba la Burigi, ambapo pamoja na mambo mengine, atakabidhi vibali na hati kwa wawekezaji mbalimbali ili kuwekeza katika eneo hilo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla amesema hayo jijini Mwanza jana, katika mkutano wa mwaka wa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa).

Alisema ili sekta ya hifadhi iweze kuleta mabadiliko ni lazima jamii wakiwamo wanahabari washiriki katika kutangaza vivutio vya utalii kama njia ya kuongeza idadi ya wageni wa ndani na nje.

“Bila wanahabari sekta ya utalii haiwezi kujulikana hivyo tushirikiane pamoja katika hili.

“Na pia kama mnakumbuka hivi karibuni tumetangaza hifadhi mpya za taifa na Jumanne Rais Magufuli, atazindua hifadhi ya Burigi Chato, lengo ni kuhakikisha wageni waweze kuona maliasili zetu popote pale Tanzania,” alisema Dk. Kigwangalla.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger