Saturday, 20 July 2019

Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi sikukuu ya Nanenane

...
Rais  Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) yatakayofunguliwa na Makamu wa Rais mkoani Simiyu.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema baada ya ufunguzi utakaofanywa na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, pia Agosti 3, mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atatembelea maonesho hayo yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi.

“Kwa taarifa hii, napenda kutoa mwito kwa wadau wote wa sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, ushirika, maliasili na mazingira pamoja na wananchi wote kushiriki kwa dhati katika maonesho ya mwaka huu,” alisema Hasunga.

Waziri Hasunga aliwataka wadau kuzingatia kwamba mahudhurio yao yatakuwa ya manufaa kwani watajionea mbinu za kuboresha shughuli mbalimbali zinazowahusu wanunuzi na wafanyabiashara watapata fursa ya kutangaza bidhaa zao kwenye maonesho hayo yatakayoanza Agosti Mosi hadi Agosti 8 katika kanda zote nane.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

FUNGUA PAZIA

NDOA ZA UTOTONI

Narudi nyumbani

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger