NA SALVATORY NTANDU
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linaendelea na uchunguzi wa tukio la kifo cha Maganga Shija (42) mkazi wa kijiji cha Galamba aliyekutwa akiwa amefariki dunia katika eneo la daraja lililopo barabara ya Shinyanga mjini kwenda Galamba.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Richard Abwao ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na waandshi wa habari ofsini kwake na kusema kuwa mwili wa Maganga uliokotwa katika eneo hilo julai 8 mwaka huu ambapo taarifa zinaonesha alitoka katika kijiji hicho kwenda kijiji jirani.
Amesema Marehemu aliaga nyumbani kwake anakwenda kuangalia mchezo wa ngoma za kienyeji katika kijiji cha Nobora Kata ya Ukenyenge wilaya ya kishapu julai 3 lakini hakuweza kurudi hadi alipokutwa akiwa amefariki dunia katika daraja hilo.
Kamanda Abwao amesema kwa sasa jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo cha kifo cha Marehemu.
0 comments:
Post a Comment