Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam (SACP) Lazaro Mambosasa, amewataka watu wenye taarifa zitakazosaidia upatikanaji wa Raphael Ongangi, waziwasilishe ofisini kwake ili zifanyiwe kazi.
Akizungumzia juu ya kauli zilizotolewa na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe juu ya alipo Raphael, kamanda amesema taarifa hizo ni za mitandaoni, na kwamba wao hawafanyii kazi mambo ya mitandao.
“Hizo habari za mitandao kila mmoja anatoa anavyofikiria, cha msingi ambacho sisi tungeweza kukiona cha maana kama kuna jambo lolote lipelekwe kituo cha polisi, ofisi yangu ipo, kama kuna mtu ana taarifa alete". alisema Mambosasa.

Siku ya Julai Mosi, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, aliahidi kuwasilisha ushahidi wa eneo alilowekwa Raphael, kuanzia siku ya kwanza alipotekwa hadi siku ya Jumamosi.
Raia huyo wa Kenya ambaye ana mke na watoto wawili, alitekwa Juni 24 maeneo ya Oyserbay Dar es salaam ambapo hadi sasa bado hajapatikana.
0 comments:
Post a Comment