Wednesday 17 July 2019

Kampuni Inayodaiwa Kumpiga Miss Shinyanga Yafungiwa Na Basata

...
Baraza la Sanaa la Taifa BASATA limeisimamisha Kampuni ya Makumbusho Entertaintment pamoja na viongozi wake kujishughulisha na shughuli yoyote ya masuala ya sanaa na burudani.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza ikieleza kuwa wakiwa kama wasimamizi wa shughuli za sanaa nchini na kupokea kwa masikitiko taarifq za unyanyasaji wa Kijinsia uliofanywa na kampuni hiyo dhidi ya mmoja wa washiriki wa Shindano la Miss Shinyanga 2019.

Tukio hilo la udhalilishwaji kwa mlimbwende Nicole Emmanuel lilifanyika Julai 6 mwaka huu Mkoani Shinyanga. BASATA imetoa wito kwa wasanii, wadau na waandaaji wa shughuli za sanaa nchini kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu zilizopo ili kulind, kuthamini na kuikuza sanaa yetu nchini.

Inadaiwa kuwa Nicole amedai kupigwa na kuchaniwa nguo hadharani na waandaji wa mashindano hayo wa Kampuni ya  Burudani ya Makumbusho Entertainment mjini Shinyanga wakati akidai fedha zake nauli shilingi 70,000/=  akiwa na mshiriki mwenzake wa shindano hilo aitwaye Agnes Masunga walipofika kwenye hoteli hiyo(kambi waliyokuwa wanaitumia) ili kudai nauli zao.

Waandaji wa Shindano hilo wanaotuhumiwa kumpiga na kumdhalilisha binti huyo ni Meneja Mkuu wa Makumbusho Entertainment,George Foda na Mkurugenzi wa Makumbusho Entertainment Richard Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU) mkoa wa Shinyanga.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger