Monday, 1 July 2019

Afcon 2019: Taifa Stars Kuvaana na Algeria Leo

...
Timu  ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, leo inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Algeria katika mchezo wa tatu wa Kundi C wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019), inayoendelea jijini Cairo nchini Misri.

Michuano hiyo ambayo ilianza Juni 21 na kutarajiwa kumalizika Julai 19, mwaka huu, nchini humo, timu ya Tanzania haina matumaini ya kutinga hatua ya 16 bora, hata kama itashinda dhidi ya Algeria, baada ya kuanza vibaya.

Hilo linatokana na Taifa Stars kupoteza michezo miwili dhidi ya Senegal na Kenya, ambayo ilifungwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Senegal, kisha kupigwa mabao 3-2 na jirani zao Kenya.

Kwa matokeo hayo, mchezo wa leo kwa Taifa Stars utakuwa wa  kukamilisha ratiba ya michuano hiyo  kutokana na kutofanya vizuri michezo yake miwili.

Taifa Stars iliyofanikiwa kufuzu michuano hiyo, baada ya kuifunga Uganda  mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano uliochezwa Machi 24, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, imeonekana kushindwa kuhimili mikikimikiki ya Afcon .

Matokeo hayo yaliifanya Tanzania kumaliza nafasi ya pili Kwa kutoka Kundi L, kutokana na pointi,  nyuma ya Uganda aliongoza kundi hilo kwa pointi 13, Lesotho ilimaliza nafasi ya tatu kutokana na pointi sita na Cape Verde ilishika mkia kwa  pointi tano.   

Historia ya timu ya Tanzania  kufanya vibaya Afcon inajirudia baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria kushika mkia katika Kundi A, lililoundwa na mwenyeji, Misri na Ivory Coast.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger