MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Njombe Scolastika Kevela ameunga mkono hatua ya uongozi wa CCM Taifa kwa kuwapongeza wafanyakazi kwa tamko lao la kuunga mkono kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa kuhusu nyongeza ya mshahara.
Ametoa kauli hiyo wakati wa akiwatakia salamu za Idd wananchi wa Mkoa wa Njombe na watanzania wote ambapo alisisitiza kuwa kitendo kilichofanywa na Chama chake kupitia kwa Katibu Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka kinaonesha namna gani chama hicho kinazingatia masuala ya utu.
"CCM ni Chama cha watu na chenye kujali Utu, kitendo cha uongozi wa juu kuwapongeza wafanyakazi kwa kuunga mkono kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu suala la Ongezeko la mishahara kinastahili pongezi" amesema Mama Kevela
Awali chama hicho kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wake wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka iliwapongeza wafanyakazi hao chini ya Shirikisho la wafanyakazi(TUCTA) kwa tamko lao la kuunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan juu ya nyongeza ya mshahara alilolitoa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Mkoani Dodoma 1 Mei 2022.
"Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA amesema walikutana na Rais siku moja kabla ya sherehe za Mei Mosi na kukubaliana juu ya ajenda hiyo ambapo Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliwahakikishia kuwa serikali itapiga mahesabu na nyongeza hiyo itapatikana katika mwaka mpya wa fedha unaoanza mwezi wa Julai 2022" alisema Shaka kupitia taarifa yake.
Katika taarifa yao TUCTA pia imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa hatua hiyo lakini hatua yake ya kukubali wafanyakazi waliyofukuzwa kazi baada ya kukutwa na vyeti bandia walipwe stahiki zao, kitendo ambacho kimedhihirisha wazi namna Rais Samia Suluhu Hassan alivyokuwa muumini wa Haki, huruma na mapenzi mema kwa kila mtanzania.
Aidha akizungumzia hilo, Mwenyekiti huyo wa UWT Mkoa wa Njombe amesema Chama Cha Mapinduzi siku zote kimekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha maslahi ya wananchi wake na haki zao zinasimamiwa na kulindwa hatua iliyomfanya Rais Samia umuhimu wa waliokuwa watumishi hao kulipwa stahiki zao.
Shaka katika taarifa hizo alisistiza kuwa majibu hayo ya TUCTA kuwa ni sahihi kwa wanasiasa wasio na maslahi na wafanyakazi wala nchi yetu ambao wanaumizwa na mazuri yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na wao hupenda kubadili mazuri kuwa mabaya ili wajijengee umaarufu na ushawishi wa kisiasa kwa wananchi.
Katika kipindi cha miaka mitano (2020-2025) Chama Cha Mapinduzi kiliahidi kupitia ilani yake ya uchaguzi ibara ya 130 kuwa serikali itakazoziunda zitaendelea kuweka mazingira rafiki ya utendaji wa vyama vya wafanyakazi ili viendelee kuwa nguzo muhimu katika kujenga mahusiano mahala pa kazi na kuboresha masilahi na haki za wafanyakazi ikiwemo uboreshaji wa mishahara ya watumishi wa umma ili waweze kumudu gharama za Maisha kwa kuzingatia ukuaji wa uchumi wa Taifa na tija ya wafanyakazi.
Hivyo anachokifanya Rais Samia Suluhu Hassan siyo maneno bali ni vitendo ikiwa ni utekelezaji wa ilani, Chama Cha Mapinduzi kinampongeza sana kwa umakini wake katika kuitekeleza ilani kwa vitendo.
0 comments:
Post a Comment