Thursday, 26 May 2022

MSANII SITI AMINA ATUNUKIWA UBALOZI WA UTALII ZANZIBAR

...


Na Rahma Idrisa - Zanzibar

Wizara ya Utalii na Mambo ya kale Zanzibar imemtunukia ubalozi wa utalii na mambo ya sanaa mwanamuziki wa kike kutoka Zanzibar  Omar Juma maarufu kama Siti Amina. 


Akizungumza na vyombo vya habari katika makabidhiano hayo hafla iliyofanyika katika ukumbi wa wizara hiyo Wazir Simai Mohammed Saidi amesema kuwa wizara ya utalii na mambo ya kale imempa ubalozi huo kutokana na juhudi zake kubwa za sanaa ya muziki anayoifanya.


"Wizara tumempa ubalozi huu kwanza tumemuona kuwa ni mwanamke jasiri na mwenye ushawishi mkubwa ,amekuwa akiimba nyimbo ambazo zinaitangaza Zanzibar kwa kuzingatia maadili ya mzazibar .


" Hata ivyo tunaimani naye kubwa katika kuitangaza Zanzibar hasa kupitia sanaa yake ya mziki anayoifanya " amesema.


Ameongeza kuwa Amina Omar Juma maarufu kama Siti Amina ambaye ni muhitimu wa muziki kutoka chuo cha nchi ya majahazi ataenda kutembelea nchi za nje takriban 5 lengo ni kuutangaza utalii wa Zanzibar .


" Mtu yoyote anaweza kuchaguliwa kuwa balozi lengo ni kuiwakilisha Zanzibar kupitia sekta ya utalii ambapo ubalozi huu utakuwa kwa muda wa miaka 3.


Kwa upande wake Amina Omar Juma balozi wa utalii kwa upande wa sanaa ameishukuru serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kumuona kuwa anaweza kuifanya kazi hiyo kwani wanamuziki wapo wengi .


"Shukran zangu za dhati nizipeleke kwa Rais wa Zanzibar kwa juhudi kubwa anazoendelea kuzifanya katika kuhakikisha nchi yetu inapokea wageni wengi ambao wanafika Zanzibar kwa kufanya utalii katika maeneo mbalimbali hata hivyo naipongeza wizara ya utalii na mambo ya kale kwa kuniamini ahadi yangu ni kuwa nitakuwa balozi mzuri na wa mfano katika kuhakikisha Zanzibar inapokea wageni wengi" , amesema.


" Aidha ameipongeza wizara ya utalii kwa kuwashika mkono wasanii wa Zanzibar na kuthamini kazi mbali mbali wanazozifanya kupitia sanaa zao .


Katika hafla hio Wizara ilimkabidhi cheti balozi huyo pamoja na bendera ya Taifa ambapo nchi anazo tarajiwa kuenda ni Italia, Ujerumani, Swizland  na Spain
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger