Mwimbaji wa nyimbo za rhumba kwa lugha ya kijaluo Alvaro Ochieng amewafurahisha mashabiki wake kwa wimbo mwingine unaoitwa Hera Mbese, wimbo unaowasifu akina mama wote ambao wamewalea watoto wao kwa uadilifu na kuwafundisha maadili ambayo yamekuwa na matokeo chanya katika jamii.Msanii Alvaro Ochieng
Alvaro Ochieng hujiita kijana wa Asembo mahali ambapo alizaliwa na kukulia. Mwimbaji huyo yuko katika harakati za kufuata nyayo za magwiji waliomtangulia kama vile Ochieng Kabaseleh, Johny Junior & Musa Juma miongoni mwa wengine kwa kuendeleza urithi tajiri wa Rhumba akiwa tayari anatamba na nyimbo kama vile Tina Molli, Aggrey Papa, Velonah Achieng & sasa Hera Mbese.
Hera Mbese ni wimbo ambao unawasifu akina mama kwa vitendo vya kijushaa wanavyovifanya au kuvipitia na nafasi zinazochezwa na akina mama.Wakati mwingine waliweka au wanaweka maisha yao kwenye mstari ili kuhakikisha watoto wanapata maisha mazuri na jinsi yanavyolipa/lipwa mara tu wanapofaulu.Tazama wimbo huo pendwa hapa.
0 comments:
Post a Comment