Afisa elimu taaluma mkoa Kigoma, David Mwamalasi (katikati mwenye suti) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akikagua na kusalimiana na wachezaji wa timu ya KIUAWASA ambao waliibuka mabingwa wa kanda wa maji Cup.
Afisa elimu taaluma mkoa Kigoma, David Mwamalasi (katikati mwenye suti) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akikagua na kusalimiana na wachezaji wa timu ya KIUAWASA ambao waliibuka mabingwa wa kanda wa maji Cup.
Afisa elimu taaluma mkoa Kigoma, David Mwamalasi (katikakati) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye kwenye fainali za maji Cup zilizofanyika uwanja wa lake Tanganyika Mjini Kigoma akisalimiana na kukagua timu ya Kigoma Veteran.
Mkuu wa wilaya Kigoma Ester Mahawe (Mwenye kofia) akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kigoma Veteran wakati wa fainali ya maji Cup kwenye uwanja wa lake Tanganyika Mjini Kigoma.
Afisa elimu taaluma mkoa Kigoma, David Mwamalasi (wa pili kushoto) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye kwenye fainali za Maji Cup zilizofanyika uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma akizungumza na wachezaji wa timu zilizoingia fainali muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo huo. (Picha zote na Fadhili Abdallah)
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
TIMU ya soka ya Mamlaka ya maji safi na maji taka Kigoma imeibuka mabingwa wa wa kanda ya magharibi wa mashindano ya kombe la maji baada ya kuifunga timu ya Kigoma Veteren kwa jumla ya magoli 6 – 1.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma washindi walijihakikishia nafasi yao tangu kipindi cha kwanza ambapo walitoka mapumziko wakiwa wanaongoza kwa magoli 3-0.
Mashindano hayo yanaandaliwa na Wizara ya maji kwa kushirikiana na Taasisi inayojishughulisha na usimamizi wa usambazaji maji nchini (ATAWAS) kwa kushirikiana na mamlaka za maji za majiji na halmashauri.
Timu ya Maveteran watabidi wajilaumu kwa wachezaji wake kushindwa kufunga licha ya kupata nafasi nzuri ya kupata magoli na hivyo kuambulia goli moja la kufuta machozi huku timu ya Mamlaka ya maji ikizidi kuongeza magoli ambapo hadi mpira unamaliza Mamlaka ya maji Kigoma Ujiji ilikuwa mbele kwa magoli 6-1.
Ushindi huo unaifanya timu hiyo ya mamlaka ya Maji Kigoma Ujiji kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya Taifa ya kombe la maji linalohusisha mamlaka za maji za mikoa nchi njema na Mamlaka hiyo ilikuwa icheze mchezo huo na timu ya mamlaka ya maji Rukwa ambayo haikutokea uwanjani.
Akizungumzia mashindano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na maji taka Kigoma Ujiji, Jones Mbike alisema kuwa yanalenga kuhamasisha jamii kushiriki kutoa taarifa ya mivujo ya maji ili kuzuia kupotewa kwa maji ambayo yamesafisha.
Mbike alisema kuwa ujumbe wa mashindao hayo pamoja na kuwa ni burudani lakini yanatumika kuimarisha afya za watumishi wa mamlaka hiyo sambamba na kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na masuala ya maji.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayosimamia usambazaji maji (ATAWAS) Constantine Chiwalo alisema kuwa kufanyika mashindani hayo kunalenga kuwakuwasanya wananchi na kupeleka ujumbe kushiriki kwenye mipango na utekelezaji wa miradi ya maji.
Chiwalo alisema kuwa mashindano hayo yanalenga pia kutoa ujumbe kwa jamii kuwa walinzi wa miundi mbinu ya maji dhidi ya wahujumu wa miundo mbinu hiyo sambamba na kusaidia kutoa taarifa kuhusu upotevu wa maji (mivujo) kwenye maeneo yao.
Afisa elimu taaluma mkoa Kigoma, David Mwamalasi akimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amezitaka mamlaka za mkoa huo kutumia michezo na burudani kufikisha ujumbe kwa wananchi kuhusu taarifa za utekelezaji wa miradi ya maji lakini pia kuhimiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji miradi, kulinda miundo mbinu na kutoa taarifa za mivujo ya maji.
0 comments:
Post a Comment