Tuesday, 24 May 2022

WADAU WA UTALII TUMIENI FURSA YA MIKOPO ILI KUHIMARISHA MAZINGIRA YA VIVUTIO NCHINI" Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii

...
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Dkt Francis Michael watatu kutoka kushoto  wakiingia kwenye kongamano la kimtandao la utalii,lililowakutanisha wadau wa utalii na Taasisi ya kifedha ya NMB na kufanyika jiji Arusha.

****************

Agness Nyamaru,Arusha.

Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na Utalii,Dkt Francis Michael amewataka wadau wa utalii mkoani Arusha kutumia fursa za mikopo nafuu ya Taasisi ya fedha(NMB) katika kuwekeza katika sekta ya utalii ili kuvutia wageni nchini.

Akizungumza katika kongamano la kimtandao la utalii(tourism Networking)Dkt.Michael alisema benki ya NMB imekuwa chachu katika kuhakikisha inawapa mikopo wadau wa sekta ya utalii katika kuhimarisha mazingira ya vivutio nchini.

"Tunaomba mfanye jitihada za kuijenga sekta ya utalii kwani serikali imeshaweka mazingira ya kuitangaza kupitia filamu ya The Royal Tour Tanzania hivyo kama wadau ni vyema mkatumia fursa hiyo katika kuweka mazingira sawa,"alisema Dkt.Michael.

Aidha aliwasisitiza wadau hao kutumia benki ya NMB katika kuhimarisha ulinzi na usalama wa watalii ikiwemo vituo vya polisi hivyo ni vyema wadau hao wakaongeza juhudi katika kuongeza idadi ya wageni nchini pamoja na kuwahudumia ipasavyo.

Naye Mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Mrisho Gambo alisema ni vyema NMB ikaongeza muda kwa wateja wao waliokopa katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa covid 19 kuwaongezea muda marejesho pasipokuwa na riba.

Kwa upande wake Afisa mkuu wa biashara na wateja binafsi wa NMB Filbert Mponzi alisema benki hiyo wanaendelea kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita kupitia Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania,Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia alisema uhitaji wa watalii wengi nchini imeongeza chachu katika kujiandaa kupitia Taasisi ya benki ya NMB kwa kuunga mkono watoa huduma katika sekta ya utalii kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi katika kuwapokea watalii nchini.

Mponzi alisema kuwa kwa miaka ya hivi karibuni wameanza kutoa huduma ya mikopo katika sekta ya utalii lengo ni kuhimarisha katika kutoa huduma kwa wageni wanaofika nchini kutalii na kuona vivutio vilivyopo nchini.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger