Monday, 30 May 2022

SHABIKI KINDAKINDAKI WA YANGA AFARIKI KWA FURAHA AKISHANGILIA USHINDI WALIVYOIBUTUA SIMBA SC

...

Feisal Salim ‘Fei Toto’ akishangilia bao alilofunga dhidi ya Simba SC
Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Simba SC katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azama Sports
 ***

NI VILIO na Simanzi vikitawala nyumbani kwa James Mhamba mwenye umri wa miaka zaidi ya Sitini ambaye alikuwa shabiki wa timu ya Yanga na mkazi wa Rwamishenye iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambaye amepoteza maisha baada ya mechi ya simba na Yanga huku chanzo kikidaiwa kuwa ni furaha baada ya timu yake kuibuka na ushindi.


Mechi hiyo ilichezwa juzi Jumamosi, Mei 28, 2022 katika Dimba la CCM Kirumba Mwanza ambapo Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ na kuipeleka Yanga Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.


Wakizungumza msibani hapo, majirani na marafiki wa mzee huyo wamesema;


“Mzee Mhamba alikuwa kiongozi kwenye umoja wetu wa Simba na Yanga (YASI), alikuwa shabiki mzuri wa Yanga, ni mtu aliyekuwa amehamasika na timu yake. Yanga ikishindwa alikuwa ananyong’onyea lakini ikishinda anachangamka sana.


Mimi nilionana naye jana kabla ya mechi alikuwa mzima tu, lakini leo nikapigiwa simu kuwa amekufa sikuamini kabisa, nimefika hapa nyumbani nikakuta kweli ameshafariki, basi tukafanya taratibu za kuupeleka mwili mochwari. Inasikitisha sana.

Alikuwa mcheshi sana na Sahabiki kindakindaki wa Yanga, ana rekodi za Yanga atakutajia wachezaji na rekodi za timu yake, sio shabiki lakini mpira alikuwa anaufahamu. Ilikuwa lazima avae jezi ya yanga, hivyo unaweza kuona alivyoipenda timu yake,” Hamidu Abdinul, mkazi wa eneo hilo.


Alikuwa na maradhi ya presha, baada ya mchezo wa jana (Simba vs Yanga), furaha ilizidi, huenda presha ilipanda ikasababisha kifo chake, amekuwa akinifundisha mengi ya kiuongozi katika chama chetu hiki, nilionana nae jana wakati wa mechi yeye akawa anaangalia kwake mimi nikaenda sehemu nyingine.


Wanasema baada ya mechi alitoka eneo alilokuwa akiangalia akaingia ndani, akavua shati lake akidai kuwa anahisi joto, akaenda kwenye bomba kujimwagia maji ya baridi, hapo hapo ndipo alianguka chini, wakaita majirani, lakini walipokuwa wakimuingiza ndani wakagundua tayari ameshakufa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger