Saturday, 28 May 2022

WAWAKILISHI WA JAMII YA WAFUGAJI NGORONGORO WAIOMBA SERIKALI KUFANYIA KAZI RIPOTI WALIYOIWASILISHA SERIKALINI

...


Na Rose Jackson - Arusha.

Wawakilishi wa jamii ya Wafugaji wa tarafa ya Loliondo wamewasilisha serikalini ripoti na mapendekezo ya jamii yanayohusu tarafa ya Loliondo ambapo wameomba serikali kuisoma ripoti hiyo kwanza ndipo wakae na kamati hiyo ili waweze kujadiliana waliyokubaliana.


Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji wilayani Ngorongoro ambaYe ni mjumbe wa kamati iliyoandaA ripoti hiyo Edward Maura akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ripoti hiyo amesema kuwa ripoti na mapendekezo waliyoiwasilisha serikalini.


Amesema kuwa wanategemea kuwa mara baada ya kukabidhi ripoti hiyo wanaamini serikali itaisoma kwanza na ndipo wakutane na jamii na kamati hiyo kwa ajili ya makubaliano.


"Waziri mkuu alitoa fursa kwa wananchi wa tarafa ya Loliondo na Ngorongoro kuandika changamoto za ongezeko la watu na Changamoto ya kilomita 1500 iliyoko Loliondo na sisi tulikubali kukaa na kuunda kamati mbili ya tarafa ya Loliondo na tarafa ya Sale na bahati nzuri Wananchi walitoa ushirikiano na tumeweza kuiwasilisha serikalini",aliongeza Maura.


Amemwomba waziri mkuu kuangalia mambo yanayoendelea Ngorongoro ya baadhi ya watu kuhamishwa kwenye mamalaka ya hifadhi ya Ngorongoro ya vijana kumi wanaotoka eneo hilo na kuiomba serikali kuangalia uhamisho huo kama umezingatia kanuni na sheria .


Aidha wamemshukuru waziri mkuu kupokea mapendekezo hayo na kuiomba serikali kusoma kwanza ripoti hiyo na haitafanya Jambo lolote bila kukaa na kuzungumza kwa pamoja.


Naye Mwenyekiti wa kamati ya uandaaji wa ripoti hiyo tarafa ya Ngorongoro , Metui Oleshaudo amesema kuwa kazi waliyoifanya ya kukusanya maoni kwa kata zote za wilaya ya Ngorongoro wameshamaliza na wameifikisha serikalini na wanaiomba serikali ifanyie kazi ripoti hiyo .


Kwa upande wake Magreth Kaisoi kutoka tarafa ya Ngorongoro amesema kuwa waziri mkuu aliagiza kamati kukusanya maoni ya wananchi kutoka nanja tatu ambayo ni ongezeko la watu, ongezeko la mifugo pamoja na ujenzi holela ambapo amedai kuwa ripoti hiyo ikisomwa vizuri serikali itaweza kuelewa uhalisia .


Mapendekezo hayo yaliyokabidhiwa na kamati hiyo serikalini ni maoni ya wananchi ambao hawaami Ngorongoro ambapo waziri mkuu alitoa maelekezo kwa jamii hiyo kuunda kamati ya kuandika maoni na mapendekezo ya changamoto za tarafa ya Sale na Loliondo ili serikali iweze kuyatafutia uvumbuzi.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger