Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Murilo Jumanne Murilo
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini
UCHUNGUZI uliofanywa na Vyombo vya Dola umebaini kuibuka kwa baadhi ya wanawake wanaofundishana kufanya matendo ya ngono kwa kutumia vifaa hatarishi kama chupa za bia soda, mahindi ya kuchoma, ndizi na matango.
Baadhi wameunda makundi ya WhatsApp ili kuweka picha zao za utupu na wengine huziweka katika mitandao tofauti ya kijamii. Uchunguzi zaidi umebaini kuwa wanawake na mabinti wanaoonekana kukubuhu kufanya vitendo hivyo husafirishwa kwenda ughaibuni na kutumikishwa katika biashara ya ukahaba, jambo ambalo ni kinyume cha Sheria za Nchi yetu.
Kufuatia kuendelea kufanyika kwa matendo hayo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika Hotuba yake tarehe 03, Mei 2022 alipokuwa akifungua Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwa Bara la Afrika Jijini Arusha,aliguswa sana na kuporomoka kwa maadili.
Alitumia jukwaa hilo kuelekeza viongozi kusimamia suala la Maadili nchini. Kufuatia Maelekezo hayo ya Mhe, Rais, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alizielekeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wanawake Wazee, na Makundi Maalum kushirikiana kukabiliana na uovu huo.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake Wazee na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Vyombo vya Dola, zimefanikiwa kuwanasa jumla ya wanawake na mabinti 16 wa mtandao unaojihusisha na Matendo maovu ya kufanya ngono kwa kutumia vifaa hatarishi kama chupa za soda na bia, mahindi ya kuchoma, ndizi na tango.
Watu hao wamekamatwa kutoka maeneo tofauti ya Mkoa wa Dar es Salaam, yakiwemo Mwananyamala, Kinondoni, Mkwajini, Tandale, Sinza, Buza na Magomeni. Aidha, Vyombo vya dola na Mamlaka husika vinaendelea kukamilisha Taratibu za kisheria ili wafikishwe mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.”
0 comments:
Post a Comment