Baadhi ya wanawake wakiwa kwenye mazishi Geita
**
Wanawake katika kijiji cha Imaramawazo mtaa wa Ibongo kata ya Ludete wilayani Geita wamesusiwa kuchimba kaburi na kufanya mazishi ya Zawadi Mchele mkazi wa kijiji hicho aliyefariki kwa kuugua ghafla, huku wanawake hao wakihusishwa na tuhuma za mauaji ya wanaume katika kijiji hicho.
EATV imefika kijijini hapo na kuzungumza na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo la wanawake kuchimba kaburi ambapo wamesema kwamba, wanawake hao walisusiwa zoezi hilo baada ya kuhusishwa na imani za kishirikina ambapo wanaume wengi wamekuwa wakifariki bila kuugua ikilinganishwa na wanawake kijijini hapo.
"Leo wanawake ndio wamechimba kaburi, na hii inatokana na kwamba wanaume wamechoshwa na matukio ya wanaume pekee kufaliki ghafla wakati mwingine hata bila kuugua. Kwahiyo hii imefanywa kwama adhabu kwa wanawake kwamba kama wanaua basi waajibike kufanya mazishi"- Eunice Mabula, Mkazi wa Kijiji cha Imaramawazo.
Aidha, mwenyekiti wa mtaa huo Coronel Petro anasema alishangaa kupigiwa simu za jeshi la Polisi juu ya sintofahamu ya wanaume kwenye kijiji hicho kutoshiri mazishi ndipo yeye pamoja na Jeshi la Polisi wakafika kwenye kijiji hicho na kuwaamuru wanaume kijijni hapo kushiriki mazishi.
Hata hivyo, baada ya Jeshi la Polisi kuamuru mazishi yafanywe na wanaume, wakazi wa mtaa huo (wanaume) kwa kushirikiana na wanawake kutoka kijiji cha jirani wakafanikisha mazishi hayo ambayo wanawake wa kijiji husika hawakushiriki kutokana na kuogopa kususiwa tena mazishi.
CHANZO - EATV
0 comments:
Post a Comment