Sunday, 29 May 2022

TBS YATOA ELIMU YA UDHIBITI UBORA KWENYE MAONESHO YA TATU YA FAHARI YA GEITA

...

******************************

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki katika Maonesho ya Tatu ya Fahari ya Geita yanayoendelea mkoani Geita ambayo yamejumuisha wazalishaji wa bidhaa mbalimbali wanaopatikana mkoani humo pamoja na mikoa ya jilani.

Akizungumza leo Mei 29,2022 katika Maonesho hayo, Afisa Usalama wa Chakula Mkuu TBS Kanda ya Ziwa Bw.Julius Panga amesema lengo la maonesho hayo ni kuona namna gani bidhaa mbalimbali zinavyozalishwa na wajasiriamali wa mkoa huo na kutoa elimu ya udhibiti ubora wa bidhaa hizo.

Amesema kupitia maonesho hayo wameendelea kutoa elimu kwa wananchi pamoja na wazalishaji wa bidhaa kufahamu majukumu makubwa yanayifanywa na TBS pamoja kuona ni namna gani wanaweza kuzalisha bidhaa zenye viwango vinavyotakiwa.

"Tumekuwa tukiwajukisha majukumu ya Shirika na kuonana na wajasiriamali ambao wanahitaji huduma ya Shirika pamoja na kufahamu namna ya kupata alama ya ubora kwenye bidhaa". Amesema Bw.Panga.

Aidha amewataka wazalishaji,waandaji wa bidhaa na wananchi kwa ujumla kutembelea kwenye maonesho hayo ili waweze kupata elimu ya kutosha kuhusu majukumu ya TBS.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger