Saturday, 28 May 2022

Utafiti : HAKUNA POMBE ISIYOKUWA NA MADHARA....HATA KAMA NI GLASI MOJA TU

...


Habari mbaya kwa wale ambao huwa wanafurahia na kufikiri kwamba bilauri moja ya mvinyo kwa siku ni nzuri kwa kiafya.


Utafiti mkubwa uliofanywa duniani na kuchapishwa katika jarida la lancet umethibitisha kwamba utafiti uliofanywa awali na kuonyesha kwamba hakuna usalama katika unywaji wa pombe.

Watafiti wamekubali kwamba kunywa kwa kiasi kunaweza kumlinda mtu dhidi ya ugonjwa wa moyo lakini waligundua kwamba kuna hatari ya mtu kupata saratani na kukosa kinga ya magonjwa mengine.


Mwandishi wa utafiti huu alisema matokeo aliyoyapata yalikuwa ya muhimu sana kwa sasa kwa sababu ya mambo mengi yaliyozingatiwa


Je! unywaji wa pombe unasababisha hatari kubwa kwa kiasi gani?


Utafiti uliofanywa na 'Global Burden of Disease'unaangalia kiwango cha pombe na madhara yake kiafya kwa mataifa 195 ikiwemo Uingereza katika miaka ya 1996 mpaka 2016.


Utafiti uliangalia umri kuanzia miaka 15 hadi 95,mtafiti alilinganisha watu ambao wanakunywa pombe hata chupa moja kwa siku na wale ambao hawanywi kabisa.


Na kubaini kwamba watu wasiokunywa kati ya 100,000 ni watu 914 tu ndio wanasumbuliwa na matatizo ya kiafya kama saratani au kusumbuliwa na majeraha yeyote.


Lakini watu wanne zaidi wanapata madhara kama wanakunywa pombe hata chupa au bilauri moja kwa siku.

Maelezo ya picha,

Imethibitishwa kwamba hakuna pombe iliyo na manufaa kiafya


Kwa watu ambao hunywa chupa mbili za pombe kwa siku,Watu 63 kati yao uanza kupata mabadiliko ya kiafya na wale ambao hutumia chupa tano kwa kila siku kuna ongezeko kubwa la watu wapatao 338 ambao hupata madhara ya kiafya.


Kiongozi wa tafiti hiyo Dr Max Griswold kutoka Taasisi ya Health Metrics and Evaluation (IHME) katika chuo cha Washngton alisema kwamba utafiti wa awali ulibaini kwamba kuna hatari kubwa za kiafya ambazo zinahusishwa na uongezekaji wa uywaji wa pombe.


Uhusiano mkubwa wa matumizi ya pombe na hatari ya kupata saratani pamoja na magonjwa ya kuambukiza inaondoa kinga ya ugonjwa wa moyo katika utafiti.


Je, unakunywa pombe kiasi gani?

Ingawa hatari ya matumizi ya pombe huanza polepole hukua kwa haraka kwa watu ambao hunywa pombe kwa kiwango kikubwa.


Mwaka 2016 ,serikali Uingereza iliweka kiwango ambacho watu wnapaswa kutumia kwa wanawake na wanaume ili kupunguza athari ya ongezeko la ugonjwa huo.

Chanzo - BBC SWAHILI

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger