Friday, 13 May 2022

WAZIRI WA MAJI JUMAA AWESO ATINGA BUNGENI NA WAKE ZAKE WAWILI.....'HAYA NI MAHABA MAZITO SANA'

...

Waziri wa Maji Jumaa Aweso, akiwa na wake zake
**
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amesema kwamba ushirikiano anaopewa na wake zake wawili hauoneshi tu kama ni mapenzi bali ni mahaba mazito na kwamba hata kuchakarika kwake kunatokana na ukaribu wao kwake.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 12, 2022, Bungeni Dodoma, wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2021, ambapo wake zake wote wawili wamehudhuria bungeni kumshuhudia.

"Leo wake zangu wote wawili wamekuja hapa kuni-support haya sio mapenzi haya ni mahaba mazito sana, mimi ninawapenda sana ukiniona nachakarika ni kwa sababu ya ukaribu wao na ushirikiano mkubwa wanaonipa, mimi Jumaa Aweso nitaendelea kuwapenda sana wake wangu," amesema Waziri Aweso.

Chanzo - EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger